Inajengwa sasa

Umepost mzigo. Oda zinamiminika. Hakuna inayopotea.

SUHU Mauzo inasoma kila ujumbe wa WhatsApp, inajibu bei, upatikanaji na gharama ya usafirishaji yenyewe, na inaingiza kila oda kwenye orodha moja — bidhaa, size, idadi na eneo. Wewe unapakia tu.

Hii ni sehemu ya SUHU — mfumo unaotumika tayari na biashara Tanzania kwa ujumbe na simu za WhatsApp. Sehemu ya oda inajengwa sasa.

NM
Neema M.mteja mpya · +255 7XX XXX XXX
Nataka ile dress ya red niliyoiona, size M. Niko Mbezi Beach10:12
SUHU IMESOMA ODA
Ipo. Dress red size M ni TZS 45,000, usafirishaji Mbezi TZS 3,000. Jumla TZS 48,000. Nithibitishe nikuwekee?10:12
Ndiyo, nithibitishie10:13
Oda #1042 Imethibitishwa
Bidhaa
Dress red · M
Idadi
1 · zimebaki 3
Eneo
Mbezi Beach
Jumla
TZS 48,000
Unajua hali hii

Mzigo mpya ni furaha — mpaka simu ianze kulia

Ujumbe mia mbili ndani ya saa moja, wote wanauliza vitu vinne vilevile. Unajibu wa kwanza hamsini, waliobaki wanachoka na kuondoka.

Maswali yale yale, mara mia

“Bei?” “Ipo?” “Size gani zipo?” “Mnafika Tegeta?” — jibu ni lile lile kila mara, lakini linaandikwa upya kila mara.

Oda zinapotea kwenye mkondo

Mtu alisema ananunua saa nne asubuhi, ujumbe umezikwa chini ya mia moja mingine. Ukikumbuka jioni, keshanunua kwingine.

Huna uhakika kilichobaki

Unauza kitu ambacho kimeisha, au unakataa kuuza kitu ambacho kipo. Vyote viwili vinaumiza — cha kwanza zaidi.

Jinsi inavyofanya kazi

Wewe unaweka mzigo. SUHU inashughulikia mazungumzo.

1

Weka bidhaa zako

Jina, bei, picha, size na rangi zilizopo, na idadi. Unaweza kuiweka kutoka simuni, na kubadilisha idadi wakati wowote.

2

Post kama kawaida

Instagram, WhatsApp Status, TikTok — popote unapouza. Wateja wanakutumia ujumbe kwenye namba yako ile ile.

3

Oda zinajipanga zenyewe

SUHU inajibu bei na eneo, inanasa oda, inapunguza idadi iliyobaki, na inakupa orodha moja: nani, nini, wapi, kiasi gani.

Uwezo

Kila kitu kinachohitajika kuuza kwa WhatsApp

Juu ya kile SUHU inachofanya tayari — inbox ya pamoja, simu za WhatsApp, na historia ya kila mteja.

📦

Katalogi na idadi halisi

Kila bidhaa na size, rangi na idadi iliyobaki. Ikiisha, SUHU haisemi ipo — inasema imeisha na inampa mteja mbadala.

🧾

Oda zinanaswa kutoka maandishi

“Ile blue size 40, mbili, Kariakoo” inakuwa oda kamili: bidhaa, size, idadi, eneo na jumla — bila wewe kuandika chochote.

🛵

Maeneo na gharama za bodaboda

Weka maeneo yako na bei zake mara moja. Mteja akitaja eneo lake, jumla inakuwa sahihi papo hapo.

📋

Bodi ya oda

Mpya, zimethibitishwa, zimefungashwa, zimetumwa, zimelipwa. Unajua zilizobaki kupelekwa leo bila kupitia mazungumzo.

💬

Mteja anajibiwa mara moja

Saa nne usiku, wakati unapakia, wakati upo njiani. Hakuna anayesubiri majibu hadi kesho — na hakuna anayeondoka kwa kukosa jibu.

📊

Ripoti ya siku

Kimeuzwa nini, kimebaki nini, wateja wangapi hawakukamilisha oda, na kipi kinahitaji kuagizwa upya.

⚠️

Kitu kimoja tunakichukulia kwa uzito

AI ikisema bidhaa ipo na kumbe imeisha, mteja anapoteza imani mara moja — na hilo ni baya kuliko kutojibu kabisa.

Kwa hiyo idadi inapungua pale oda inapothibitishwa, bidhaa inayoulizwa inashikiliwa kwa dakika chache, na wewe unaweza kubadilisha idadi kutoka simuni ndani ya sekunde. SUHU haitakisii kilichopo — inasoma kile ulichoweka.

Kwa nani

Kama unauza kwa WhatsApp, hii ni yako

👗 Nguo na mitumba 💄 Vipodozi 📱 Simu na vifaa 👟 Viatu 🍯 Vyakula na asali 💍 Mapambo 🧴 Bidhaa za ngozi 🏠 Vitu vya nyumbani

Unataka kuwa wa kwanza kuitumia?

Tunaijenga sasa, na tunataka kuijenga na wauzaji halisi. Tuambie unauza nini na oda zako zinakujaje — utapata kuitumia kabla ya wengine, bila malipo mwanzoni.